WAHADZABE (SWAHILI VERSION) by Peter Peterson

KShs 2,750.00

Daudi Peterson akishirikiana kwa ukaribu sana na viongozi wa Wahadzabe wa Tanzania, anatupa picha adimu, ya kweli na ya ndani ya moja ya jamii za mwisho za wawindaji-wakusanyaji ulimwenguni wanavyoiona wenyewe kwa mtizamo wao. Kwa maelfu ya miaka historia yao imetunzwa kupitia hadithi zinazosimuliwa na wazee wakiwa wamezunguka mioto isiyohesabika katika kambi zao porini katika bonde la Yaeda. Kwa uzoefu wao wa miaka miaka mingi wakifanya kazi na kufuata Wahadzabe katika mbuga zao, Daudi, Trude Peterson na Jon Cox walipiga picha na kuweka kumbukumbu ya maisha ya kila siku ya wawindaji-wakusanyaji, utamaduni na maarifa yao ya uchimbaji wa mizizi, ukusanyaji wa asali na mimea ya dawa, uwindaji wa wanyama na utengenezaji wa zana kutokana na karibu kila kitu. Historia hii yenye picha na michoro mingi na maandiko ya Wahadzabe wenyewe ni njia bunifu ya kuweka kumbukumbu ya utamaduni wa pekee wa jamii moja ambayo imebaki kati ya jamii za asili ulimwenguni.

“Wahadzabe, Kwenye nuru ya mioto milioni” ni kitabu mahsusi chenye picha ya inayovutia na kusisimua kuhusu maisha, matarajio na mitihani ya maisha ya kisasa ya Wahadzabe wanavyoyaona na kwa kauli zao wenyewewe. Sikiliza wazee wakitamba hadithi za kale. Jifunze ya kuwinda, kukusanya na kusihi kwa kutegemea ardhi kwenye mazingira endelevu. Tazama nyuso za wanaume, wanawake na watoto wa kihadzabe. Na wewe hisi uchungu wao wa kupotelewa na ardhi, rasilimali na haki zao. Peterson na washirika wake wa kihadzabe wametoa maelezo yanayovutia sana na yenye kusikitisha juu ya jamii ya wawindaji- wakusanyaji wachache ambayo imebaki hadi sasa, jamii inayojitahidi sana kuhifadhi uwezo wake wa kudumisha maisha yao na umiliki wa ardhi yao. Kitabu hiki si cha kukosa kwa mtu mwenye kupenda kufahamu kuhusu mambo ya kale, ya sasa na ya baadaye ya Afrika na waafrika.”

—Dorothy L. Hodgson, Profesa na Mwenyekiti wa Anthropolojia, Rutgers University Mwandishi wa Once Intrepid Warriors, The Church of Women, Being Maasai, Becoming Indigenous

“Daudi Peterson na washirika wake wa kihadzabe wameandika historia ya maisha na utamaduni wa kale ambao karibu umetoweka, lakini wa watu ambao bado hai. Picha wanayoonyesha inatuunganisha na maisha ya uwindaji na ukusanyaji wa mababu zetu wa Afrika kwa kuweka kumbukumbu ya jamii ya wahadzabe mia chache wanaoelewa fika umuhimu wa historia yao: watu wa kisasa ambao ni salio la mwisho la kiungo chetu na kale yetu.”

—Richard Wrangham, Mwandishi wa Catching Fire: How Cooking Made Us Human

“Daudi Peterson na washirika wake wa kihadzabe wameandika historia ya maisha na utamaduni wa kale ambao karibu umetoweka, lakini wa watu ambao bado hai. Picha wanayoonyesha inatuunganisha na maisha ya uwindaji na ukusanyaji wa mababu zetu wa Afrika kwa kuweka kumbukumbu ya jamii ya wahadzabe mia chache wanaoelewa fika umuhimu wa historia yao: watu wa kisasa ambao ni salio la mwisho la kiungo chetu na kale yetu.”

In stock

SKU: 9789987082452 Categories: , ,